
Ashtakiwa kwa kutapeli akidai angegeuza Sh230,000 za mfanyabiashara ziwe Dola za Kimarekani zenye thamani kubwa
NA RICHARD MUNGUTI
MWANAMUME aliyedai atafanyia muujiza na mazingaombwe sarafu za Kenya na kuzigeuza kuwa Dola za Kimarekani ndani ya Msikiti wa Jamia ameshtakiwa kwa ulaghai.
Lali Mohamed Abdi alishtakiwa mbele ya hakimu mkuu Lucas Onyina kwa kumpiga kifumbamacho Erick Shikoli Litwachi na kumpora Sh230,000.
“Shtaka linalokukabili ni kwamba mnamo Februari 17 katika Msikiti wa Jamia ukiwa na nia ya kulaghai ulimdanganya Bw Shikoli ungegeuza sarafu za Kenya alizokuwa nazo Sh230,000 kuwa Dola. Ni ukweli au sio ukweli,” Bw Onyina alimwuliza mshtakiwa.
“Sio ukweli,” Abdi alijibu.
Aliomba aachiliwe kwa dhamana akisema atakuwa anafika kortini kila anapotakiwa.
Bw Onyina alimwachilia kwa dhamana ya Sh3 milioni.
Kesi itatajwa baada ya wiki mbili kutengewa siku ya kusikilizwa.
Source link