
Barcelona wakomoa Cadiz na kufungua mwanya wa alama nane kileleni mwa jedwali la La Liga
Na MASHIRIKA
BARCELONA walitandika Cadiz 2-0 katika Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga) mnamo Jumapili ugani Camp Noun a kufungua pengo la alama nane kati yao na nambari mbili Actual Madrid kileleni mwa jedwali.
Sergi Roberto aliwaweka Barcelona kifua mbele mwishoni mwa kipindi cha kwanza baada ya kujaza kimiani mpira uliorejea uwanjani baada ya kupigwa na Robert Lewandowski na kugonga mhimili wa goli.
Lewandowski alifungia Barcelona bao la pili mwishoni mwa kipindi cha kwanza baada ya kumegewa krosi safi na Roberto.
Mechi dhidi ya Cadiz ilikuwa ya kwanza kwa Roberto na Lewandowski kuchezea Barcelona uanjani Camp Nou tangu Oktoba 23, 2022 walipoongoza waajiri wao kulaza Athletic Membership Bilbao 4-0.
Chini ya kocha Xavi Hernandez, Barcelona walipata nafasi kadhaa za kufunga mabao zaidi katika kipindi cha pili ila wakazipoteza kupitia kwa Lewandowski aliyeshuhudia kombora lake likigonga mwamba.
Lewandowski, ambaye ni raia wa Poland, sasa amepachika wavuni mabao 15 kutokana na mechi 19 za La Liga. Cristiano Ronaldo aliwahi kupachika wavuni magoli 15 kutokana na mechi 17 za La Liga mnamo 2009-10 na kuweka rekodi ya kufikisha idadi hiyo ya magoli baada ya michuano michache zaidi.
Barcelona, ambao washindani wao wakuu Actual Madrid walitandika Osasuna 2-0 mnamo Jumamosi, wameshinda sasa mechi saba zilizopita za La Liga na hawajapoteza mchuano wowote kati ya 13.
Aidha, safu yao ya ulinzi inazidi kuimarika ikiwa sasa hawajafungwa bao katika mechi 17 mfululizo. Hiyo ni rekodi mpya baada ya mechi 22 La Liga ikizingatiwa kwamba Deportivo de La Coruna waliwahi kupiga mechi 16 mfululizo ligini bila kufungwa mnamo 1993-94.
Cadiz, walioshuhudia mabao yao mawili dhidi ya Barcelona yakikataliwa, sasa wanashikilia nafasi ya 17 kwa alama 22 sawa na Almeria.
MATOKEO YA LA LIGA (Jumapili):
Barcelona 2-0 Cadiz
Elche 0-1 Espanyol
Rayo Vallecano 1-1 Sevilla
Atletico Madrid 1-0 Athletic Bilbao
TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO
Source link