
Bonde laibukia kuwa ngome maarufu ya pombe bandia
Wateja wasiojua wamekuwa wakitumia pombe hizo katika kaunti za Narok, Bomet, Kericho na baadhi ya sehemu za Kaunti ya Nakuru. Pombe hizo hazina vibandiko kutoka kwa Halmashauri ya Ukaguzi wa Ubora wa Bidhaa (KEBS), Mamlaka ya Ushuru Kenya (KRA) na hazijaidhinishwa na idara tofauti za serikali kwa matumizi ya binadamu.
Serikali inadaiwa kupoteza mamilioni ya fedha katika kipindi cha miezi sita iliyopita kupitia watu wanaokwepa kulipa ushuru, kwani biashara hiyo imekuwa ikiendelea bila kudhibitiwa.
Maafisa wa KRA, polisi na maafisa wa utawala wamelaumiwa kwa kuwaruhusu wafanyabiashara walaghai kuhudumu katika eneo hilo bila kuchukuliwa hatua zozote.
Aina hizo za pombe zinadaiwa kusafirishwa kutoka kaunti za Nakuru, Kisii, Nyamira, Kiambu na Nairobi, ambako zinatengenezwa na wafanyabiashara walaghai katika maeneo yaliyo mafichoni, ambayo ni vigumu kutambulika na wananchi
Source link