Monday, February 27, 2023
AdvertismentGoogle search engineGoogle search engine
HomeGeneral NewsChuo chafungwa wanafunzi wakidai kuvamiwa na jini – Taifa Leo

Chuo chafungwa wanafunzi wakidai kuvamiwa na jini – Taifa Leo

Chuo chafungwa wanafunzi wakidai kuvamiwa na jini

Chuo chafungwa wanafunzi wakidai kuvamiwa na jini

NA KALUME KAZUNGU

MASOMO yalisitishwa katika Chuo cha Kiufundi cha Lamu jana Jumatatu, baada wanafunzi kuzua fujo iliyodaiwa kuchochewa na majini.

Mkanganyiko ulianza mwendo wa saa nne asubuhi wakati mwanafunzi wa kike alianza kupiga kelele na kutamka maneno yasiyoeleweka.

Walioshuhudia, walisema jitihada za kumdhibiti hazikufua dafu kwani alianza kuwashambulia walimu na wanafunzi kwa ngumi na makofi.

Wanafunzi wengine watano nao walianza kutenda vivyo hivyo, wakiingia katika baadhi ya madarasa na kuwapiga wenzao.

Mkurugenzi wa chuo hicho, Bw Fidel Mulei, hata hivyo alipuuzilia mbali madai kuhusu majini akisema mwanafunzi aliyeanza kelele alikuwa amekasirishwa na wenzake.

Alisema waliamua kufunga chuo wakati wengine pia walianza fujo, lakini walitarajiwa kurudi baadaye.

Mhubiri wa Kiislamu, Bw Mahmoud Ahmed Abdulkadir, alisema tabia hizo huchochewa na saikolojia hasa baina ya wanawake, lakini huwa wanarudia hali ya kawaida baada ya muda mfupi.


Source link

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -spot_img

Most Popular

Home
News
RSS