
GUMZO: Enrique anapigiwa upatu kunoa Chelsea Potter akifurushwa
IMEKUSANYWA NA CECIL ODONGO
BRAZIL imeondoa jina la Luis Enrique kati ya wakufunzi waliokuwa wakilengwa ili kunoa timu ya taifa Samba Boys.
Hii ni baada ya kubainika kuwa huenda Enrique akachukua nafasi ya Graham Potter kambini mwa Chelsea.
Baadhi ya mashabiki wa The Blues wamekuwa wakitaka Potter aonyeshwe mlango kufuatia msururu wa matokeo duni ambayo yanaandama timu hiyo.
Licha ya kununua wachezaji wa haiba kwa kishindo mnamo Januari, Chelsea wamekuwa hoi huku mbinu za ukufunzi za Potter nazo zikitajwa kama zinazodidimiza kikosi hata wanapocheza nyumbani Stamford Bridge.
Jinsi ilivyo kwa sasa Chelsea huenda ikawa na kibarua kigumu cha kumaliza miongoni mwa timu nne bora na kufuzu kushiriki Uefa.
Enrique alijiuzulu kama kocha wa Uhispania baada ya timu hiyo kuondolewa kwenye raundi ya 16-bora ya Kombe la Dunia nchini Qatar mnamo Desemba 2022.
Akiwa kocha wa Barcelona, Enrique, 47 alishinda La Liga mara mbili: misimu ya 2014-15 na 2015-16.
Pia alishinda Copa del Rey mara mbili, Supercopa de Espana, Uefa Tremendous Cup na FIFA Membership World Cup.
Source link