
Dawa: Hofu raia wanashauriwa ndivyo sivyo
ANGELA OKETCH Na HELLEN SHIKANDA
RIPOTI iliyotolewa na Younger Pharmacists Group (YPG) wiki jana inaonyesha kwamba baadhi ya wanafamasia waliojiriwa katika hospitali za rufaa hawajahitimu.
Ripoti hiyo inaonyesha kwamba hospitali nane kati ya 10 zimewaajiri wanafamasia wasio na tajriba hitajika.
Kulingana na ripoti hiyo, huenda Wakenya wanapata ushauri usiofaa kuhusu dawa.
Utafiti huo uliofanyika katika hospitali za Ngazi ya 4 na 5 nchini pia umebaini kuwa dawa katika asilimia 70 ya hospitali za Ngazi ya 5 zinatolewa na watu waliopewa leseni na wasio na sifa za kufanya hivyo.
Utafiti uliofanywa katika hospitali 535 za Ngazi ya 4 na vituo 80 vya Ngazi ya 5 vilivyoorodheshwa kwenye tovuti ya Baraza la Madaktari wa Meno nchini ulibaini kuwa takriban vituo nane kati ya 10 (asilimia 80) vya ngazi ya 4 havikukidhi viwango hitajika.
Kati ya vituo vyote 535 vilivyojumuishwa kwenye utafiti, vituo 424 havikukidhi viwango, na 50 pekee vilizingatia viwango vinavyohitajika. Utafiti unaonyesha kuwa vituo 61 havikuwa na information hitajika.
Kadhalika, ripoti hiyo pia ilionyesha kuwa asilimia 71 ya vituo vya ngazi ya 5 havikusimamiwa na wanafamasia waliohitimu.
Kaunti ya Nairobi ilikuwa na idadi kubwa zaidi ya vituo ikiwa na asilimia 19.4, Kiambu asilimia saba, Nakuru na Kisumu asilimia 4.3 kila moja, Kajiado na Mombasa asilimia nne kila moja, Wajir asilimia 3.4, Machakos asilimia 2.4 huku Nandi ikiwa na asilimia 1.3.
Hii ni kinyume na sheria ambapo msimamzi wa dawa anafaa kuwa na leseni kutoka kwa Bodi inayosimamia dawa nchini.
Wasimamizi hao wana jukumu la kuongoza hospitali kuhusu maswala yake yote yanayohusiana na dawa ikiwa ni pamoja na kukagua faili za wagonjwa na kuwaongoza washauri wakuu kuhusu matibabu ya wagonjwa.
Msimamizi mkuu ana haki ya kukataa kutoa dawa ikiwa, kwa maoni yao ya kitaalamu, wanaona kuwa dawa hizo hazifai kwa mgonjwa.
Kutokuwepo kwa wasimamizi wakuu wa dawa kunaweka maisha ya wale wanaonunua dawa madukani hatarini kutokana na ukosefu wa tajriba.
Utafiti uliofanywa nchini Amerika ulionyesha kuwa wahudumu wa maduka ya kuuza dawa wanafaa kudhibitiwa.
“Ikiwa tutakuwa na wahudumu wa maduka ya kuuza dawa ambao hawajahitumu, basi huenda maisha ya wagonjwa yakawa hatarini. Hii ni kwa sababu wanaweza pendekeza dawa isiofaa kwa mgonjwa, jambo amablo linaweza kuhatarisha maisha ya mgonjwa,” utafiti huo ulibainisha.
Source link