Friday, February 24, 2023
AdvertismentGoogle search engineGoogle search engine
HomeGeneral NewsJeraha la kifundo cha mguu kumweka Neymar mkekani kwa kipindi kirefu –...

Jeraha la kifundo cha mguu kumweka Neymar mkekani kwa kipindi kirefu – Taifa Leo

Jeraha la kifundo cha mguu kumweka Neymar mkekani kwa kipindi kirefu

Jeraha la kifundo cha mguu kumweka Neymar mkekani kwa kipindi kirefu

Na MASHIRIKA

FOWADI matata wa Paris Saint-Germain (PSG) na timu ya taifa ya Brazil, Neymar Jr, atasalia mkekani kwa muda mrefu baada ya kupata jeraha baya la kifundo cha mguu akicheza dhidi ya Lille katika Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1) mnamo Februari 19, 2023.

Neymar, 31, aliondolewa uwanjani katika kipindi cha pili kwa machela huku akiwa amefunika uso wake kwa maumivu.

Kwa mujibu wa usimamizi wa PSG, sogora huyo wa zamani wa Barcelona atafanyiwa tathmini nyingine wiki ijayo kabla ya maamuzi ya kumfanyia upasuaji kufikiwa.

Atakosa kuwa sehemu ya kikosi kitakachotegemewa na PSG dhidi ya Bayern Munich katika marudiano ya hatua ya 16-bora ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) mnamo Machi 8, 2023 ugani Allianz Area. PSG watakuwa na kibarua kigumu cha kubatilisha ushindi wa 1-0 uliosajiliwa na Bayern katika mkondo wa kwanza wa UEFA ugani Parc des Princes.

Kufikia sasa, Neymar anajivunia kufungia PSG mabao 18 na kuchangia mabao 17 mengine katika mashindano yote. Amepachika wavuni mabao mawili na kuchangia mengine matatu katika kipute cha UEFA.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO