
Kamanda wa polisi hatarini kufurusha familia 100
NA JOSEPH OPENDA
NAIBU wa Rais Rigathi Gachagua ametangaza kwamba mkuu wa polisi Kaunti ya Nakuru atachukuliwa hatua kwa kufurusha zaidi ya familia 100.
Bw Gachagua alikuwa akirejelea aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa Nakuru, Peter Mwanzo, anayesemekana kufurusha familia 105 katika eneo la Kiriko, kaunti ndogo ya Subukia.
“Kamanda yeyote wa polisi anafaa kuarifu maafisa wa usalama wa kaunti na ujasusi kabla ya kutekeleza maagizo yoyote ya kuwafurusha watu kutoka makazi yao,” akasema Bw Gachagua.
Kadhalika, Bw Gachagua alionya watumishi wote wa umma, akisema serikali ya Kenya Kwanza itawachukulia hatua watumishi wa umma wasiofuata sheria.
Askofu Jonah Kariuki, mwenyekiti wa kampuni ya Kiriko Farmers Firm Restricted, alisema wamekuwa wakiishi katika shamba hilo kwa muda mrefu na kwamba walishangaa walipoambiwa waondoke.
Askofu Kariuki alisema kwamba hawakuhusishwa katika mchakato huo.
“Tuliambiwa tu tuhame. Hawakutuonyesha hati kutoka kwa mahakama. Hii ndio maana tutaendelea kupigania shamba letu,” akasema Bw Kariuki.
Raila, Uhuru wajipata kwenye uwanja telezi
Source link