Saturday, March 4, 2023
AdvertismentGoogle search engineGoogle search engine
HomeGeneral NewsKaunti yafadhili 300 kuhudhuria mazishi ya mzee wa jamii ya Waluo –...

Kaunti yafadhili 300 kuhudhuria mazishi ya mzee wa jamii ya Waluo – Taifa Leo

Kaunti yafadhili 300 kuhudhuria mazishi ya mzee wa jamii ya Waluo

Kaunti yafadhili 300 kuhudhuria mazishi ya mzee wa jamii ya Waluo

NA MKAMBURI MWAWASI

SERIKALI ya Kaunti ya Mombasa imewafadhili watu 300 kutoka jamii ya Waluo kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa mwenyekiti wa baraza la jamii hiyo Mzee Willis Otondi (Ker), yatakayofanyika Nyahera, Kaunti ya Kisumu leo Jumamosi.

Gavana wa Mombasa Abdulswamad Nassir, pia anatarajiwa kujiunga na waombolezaji hii leo Jumamosi, kwa mazishi hayo.

Mwenyekiti wa jamii ya Waluo eneo la Nyali, Bw Kings Obara, alisema kwamba mzee Otondi, alikuwa tegemeo kubwa kwa jamii hiyo.

Kulingana naye, alikuwa mpatanishi endapo kungeibuka vita nchini na alitoa huduma za kutafsiri mila na tamaduni za wajaluo.

“Tulimuomba gavana atusaidie ili tuweze kufika na kumpumzisha mzee wetu. Ker ni kama kuchagua pope wa kanisa la kikatoliki. Wazee huenda sehemu ya Gotramogi wanapiga kambi kama siku tatu kumteua,” alisema Obara.

Mzee Otondi alifariki Februari 17 baada ya kuugua kwa muda mrefu katika hospitali ya rufaa ya Jaramogi Oginga Odinga jijini Kisumu.


Source link

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -spot_img

Most Popular

Home
News
RSS