Saturday, February 25, 2023
AdvertismentGoogle search engineGoogle search engine
HomeGeneral NewsKhvicha Kvaratskhelia – Taifa Leo

Khvicha Kvaratskhelia – Taifa Leo

NYOTA WA WIKI: Khvicha Kvaratskhelia

NYOTA WA WIKI: Khvicha Kvaratskhelia

NA GEOFFREY ANENE

KHVICHA Kvaratskhelia ni mmoja wa wachezaji wakali kutoka taifa la Georgia hivi karibuni.

Hapajatokea mchezaji mwingine mkali kutoka taifa hilo la Bara Ulaya tangu enzi za Kakha Kaladze aliyeng’aa kati ya 2000 na 2007 akicheza kati safu ya ulinzi na pia kati.

Khvicha alitangaza kuwasili kwake katika ulingo wa soka ya kimataifa alipojiunga na Napoli inayoshiriki Ligi Kuu ya Italia kutoka Dinamo Batumi mnamo Julai 2022 kwa Sh1.5 bilioni.

Kabla ya hapo, hata hivyo, Khvicha, ambaye thamani yake imepanda hadi Sh8.0 bilioni, alikuwa ameonyesha dalili nzuri kwenye Ligi Kuu ya Urusi akichezea Rubin Kazan.

Katika msimu wake wa kwanza kwenye Serie A 2022-2023, Khvicha amepata kujumuishwa katika orodha ya wachezaji 10-bora duniani wasiozidi umri wa miaka 22.

Winga huyo amedhihirisha kuwa jarida la FourFourTwo halikukosea kumtia katika orodha hiyo kwani amechangia pakubwa katika Napoli kuwa wagombea halisi wa Serie A.

Amechana nyavu mara 10 na kusuka pasi za mwisho tisa zilizojazwa kimiani katika mechi 19 ligini.

Ana jumla ya mabao 12 na pasi 15 zilizoishia kuwa mabao katika michuano 25 kwenye mashindano yote.

Kvara, Messi wa Georgia na Kvaradona anavyofahamika kwa majina ya utani, ni stadi katika kuchanja pasi, kulisha wapinzani chenga na kufumua makombora.

Yuko sawa katika kutumia miguu yote miwili, ingawa anapenda kukata kutoka pembeni kushoto.

Mchezaji huyo ni mwerevu na mbunifu. Anajua kubadilisha kasi ya mechi.

Weledi wake umeshuhudia akimezewa mate na Newcastle United, Arsenal, Tottenham Hotspur, Manchester Metropolis, Liverpool, Actual Madrid, Chelsea na Paris Saint-Germain.

Khvicha ni mwanasoka bora wa Georgia mwaka 2020, 2021 na 2022.

Yumo mbioni kuzoa taji lake la kwanza kubwa kwani Napoli ina alama 62, 15 mbele ya nambari mbili Inter Milan baada ya mechi 23 kusakatwa.

Kimataifa, Khvicha, ambaye baba yake Badri alichezea Azerbaijan, amesakata michuano 19 tangu aanze kusakatia timu ya watu wazima ya Georgia mnamo Juni 7, 2019 akifungia magoli 10.


Source link

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -spot_img

Most Popular

Home
News
RSS