
Kocha Graham Potter asema anatishiwa maisha pamoja na ya familia yake kwa sababu ya matokeo duni ya Chelsea
NA MASHIRIKA
KOCHA wa Chelsea, Graham Potter, amesema anatishiwa maisha pamoja na ya familia yake kutokana na matokeo duni ya kikosi hicho kilichowahi kunyanyua taji la Ligi Kuu y Uingereza (EPL) mnamo 2016-17.
Chelsea wameshinda mechi mbili pekee kati ya 14 zilizopita katika mapambano yote na walipigwa na wanyonge Southampton 1-0 katika EPL mnamo Februari 18, 2023 ugani Stamford Bridge.
Usimamizi wa Chelsea umeahidi kusimama na Potter pamoja na familia yake.
“Nimepokea baadhi ya baruapepe kutoka kwa watu wasiojulikana. Wanataka nife. Bila shaka kupokea jumbe kama hizo hakufurahishi kabisa,” akasema Potter aliyeagana na Brighton mnamo Septemba 2022 na kuyoyomea Chelsea kujaza pengo la Thomas Tuchel aliyetimuliwa kwa sababu ya matokeo duni.
Potter amesema baadhi ya baruapepe ambazo amezipokea zinalenga pia kutia maisha ya watoto wake. Chini ya mkufunzi huyo, Chelsea wameshinda mechi tisa pekee kati ya 25. Kikosi hicho kwa sasa kinakamata nafasi ya 10 kwenye msimamo wa jedwali la EPL kwa alama 31 kutokana na mechi 23.
TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO
Source link