Saturday, May 27, 2023
AdvertismentGoogle search engineGoogle search engine
HomeGeneral NewsMaafisa wang’oa na kuteketeza bangi iliyopandwa kando ya barabara – Taifa Leo

Maafisa wang’oa na kuteketeza bangi iliyopandwa kando ya barabara – Taifa Leo

Maafisa wang’oa na kuteketeza bangi iliyopandwa kando ya barabara

Maafisa wang’oa na kuteketeza bangi iliyopandwa kando ya barabara

NA MWANGI NDIRANGU

MAAFISA wa usalama mjini Nanyuki, Kaunti ya Laikipia mnamo Ijumaa wameng’oa mimea 200 ya bangi iliyopandwa kando ya barabara na kuiteketeza.

Bangi hiyo ilikuwa inamea palipo na magugu mita chache karibu na duka la Cedar Mall kando ya barabara ya Nanyuki-Rumuruti.

Haikubainika mara moja ni nani aliyeipanda.

Kamishna wa Kaunti ya Laikipia Patrick Muli amesema walidokezewa kuhusu bangi hiyo kando ya barabara na walipofika hapo wakaona kweli ilikuwa inamea.

“Ni kweli tumepata bangi ikimea kando ya barabara na nikaongoza maafisa kuing’oa na kuiteketeza,” amesema kamishna Muli.

Amesema lazima kuna aliyeipanda bangi hiyo kwa sababu ili ambayo ilikuwa haijakomaa ilikuwa ikionekana kwamba ilikuwa inatunzwa.

Sehemu hiyo iko karibu na shule ya msingi.

Mzee wa kijiji Maina Njoroge amesema yeye na wanachama wengine wa mpango wa Nyumba Kumi wameanzisha hamasisho kuwataka vijana kukoma kujihusisha na uhalifu, unywaji wa pombe haramu na matumizi ya dawa za kulevya.

mwndirangu@ke.nationemdia.com