Sunday, February 26, 2023
AdvertismentGoogle search engineGoogle search engine
HomeGeneral NewsMadiwani wa zamani wamkaidi Kalonzo na kuunga serikali ya Kenya Kwanza –...

Madiwani wa zamani wamkaidi Kalonzo na kuunga serikali ya Kenya Kwanza – Taifa Leo

Madiwani wa zamani wamkaidi Kalonzo na kuunga serikali ya Kenya Kwanza

Madiwani wa zamani wamkaidi Kalonzo na kuunga serikali ya Kenya Kwanza

WAWAKILISHI wa wadi wa zamani na madiwani zaidi ya 100 katika kaunti ya Makueni wamekaidi wito wa kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka kwa viongozi wa Ukambani kutoshirikiana na Rais William Ruto.

Wanasiasa hao wakongwe kutoka vyama ya kisiasa vya Maendeleo Chap Chap, Muungano, na Wiper wamejiunga na timu ya washirika wa Rais Ruto katika eneo hilo lililopigia kura kwa wingi kiongozi wa muungano wa Azimio la Umoja One Kenya Raila Odinga katika uchaguzi mkuu uliopita.

“Tuko hapa kutangaza ili ieleweke kwamba tunamtambua Rais William Ruto kama rais halali na tutangaza kwamba tunaunga serikali yake. Tunakataa sarakasi zote za Azimio kwa sababu hazina msingi wa kisheria katika jamii yetu,” wanasiasa hao walisema katika taarifa iliyosomwa na aliyekuwa MCA wa Kasikeu Tankai Munari.

Bw Munari ni miongoni mwa wanasiasa kutoka eneo hilo ambao wameamua kuhama muungano wa Azimio walimlaumu Bw Musyoka kwa kusababisha kushindwa kwao uchaguzini na wanategemea muungano wa Kenya Kwanza utawafufua kisiasa.


Source link

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -spot_img

Most Popular

Home
News
RSS