Thursday, February 23, 2023
AdvertismentGoogle search engineGoogle search engine
HomeGeneral NewsMan-Metropolis na RB Leipzig nguvu sawa katika pambano la UEFA nchini Ujerumani...

Man-Metropolis na RB Leipzig nguvu sawa katika pambano la UEFA nchini Ujerumani – Taifa Leo

Man-City na RB Leipzig nguvu sawa katika pambano la UEFA nchini Ujerumani

Man-Metropolis na RB Leipzig nguvu sawa katika pambano la UEFA nchini Ujerumani

Na MASHIRIKA

MANCHESTER Metropolis waliambulia sare ya 1-1 dhidi ya RB Leipzig katika mchuano wa mkondo wa kwanza wa hatua ya 16-bora ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) mnamo Jumatano usiku nchini Ujerumani.

Chini ya kocha Pep Guardiola, Man-Metropolis walianza mechi kwa matao ya juu na wakamiliki asilimia kubwa ya mpira katika kipindi cha kwanza. Waliwadhibiti wenyeji wao vilivyo katika kila idara na wakafungiwa bao na Riyad Mahrez aliyeshirikiana vilivyo na Ilkay Gundogan katika dakika ya 27.

Hata hivyo, Leipzig walirejelea kampeni za kipindi cha pili kwa kishindo na nusura wasawazishiwe na Benjamin Henrichs aliyemwajibisha pakubwa kipa Ederson Moraes.

Andre Silva ni fowadi mwingine wa Leipzig aliyemshughulisha Ederson sana kabla ya Josko Gvardiol kufanya mambo kuwa 1-1 katika dakika ya 70. Kipa Janis Blaswich wa Leipzig naye alifanya kazi ya ziada na kupangua kombora zito alilovurumishiwa na Gundogan mwishoni mwa kipindi cha pili.

Man-Metropolis wanaowinda ufalme wa UEFA kwa mara ya kwanza katika historia, sasa wanapigiwa upatu wa kutamalaki Leipzig wakati wa marudiano mnamo Jumanne ya Machi 14, 2023 na kutinga hatua ya robo-fainali.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO


Source link

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -spot_img

Most Popular

Home
News
RSS