Monday, February 27, 2023
AdvertismentGoogle search engineGoogle search engine
HomeGeneral NewsMan-United wakomoa Newcastle 2-0 ugani Wembley na kutwaa ufalme wa Carabao Cup...

Man-United wakomoa Newcastle 2-0 ugani Wembley na kutwaa ufalme wa Carabao Cup – Taifa Leo

Man-United wakomoa Newcastle 2-0 ugani Wembley na kutwaa ufalme wa Carabao Cup

Man-United wakomoa Newcastle 2-0 ugani Wembley na kutwaa ufalme wa Carabao Cup

Na MASHIRIKA

MANCHESTER United walishinda taji la kwanza tangu 2017 baada ya kukomoa Newcastle United 2-0 katika fainali ya Carabao Cup ugani Wembley, Jumapili.

Maimba hao ambao sasa wamenyanyua taji la Carabao Cup mara sita tangu mwaka wa 2000, walifunga mabao yao katika kipindi cha kwanza kupitia kwa Carlos Casemiro na Marcus Rashford.

Mara ya mwisho kwa Man-United kushinda taji ni miaka sita iliyopita walipoibuka mabingwa wa Europa League na wafalme wa Carabao Cup chini ya kocha Jose Mourinho.

Walifuzu kwa fainali ya Carabao Cup muhula huu wa 2022-23 baada ya kufunga Nottingham Forest jumla ya mabao 5-0 katika nusu-fainali ya mikondo miwili huku kocha Eddie Howe akiongoza Newcastle kudengua Southampton kwa magoli 3-1.

Awali, walikuwa wamecharaza Aston Villa, Burnley, Charlton Athletic na Forest kwenye hatua za kwanza za kivumbi hicho msimu huu na kujikatia tiketi ya kuelekea Wembley kwa mara ya kwanza tangu 2017-18 walipotandikwa 1-0 na Chelsea katika fainali ya Kombe la FA.

Zaidi ya kutofungwa katika mechi tano zilizopita za Carabao Cup, Man-United pia wana fomu nzuri ya kutopigwa katika mechi 10 za mashindano yote huku wakitikisa nyavu za wapinzani angalau mara mbili katika kila mojawapo ya mechi 11 zilizopita.

Fainali dhidi ya Newcastle ilikuwa ya 10 kwa Man-United kunogesha katika kipute cha Carabao Cup ambacho sasa kimetawaliwa na vikosi vya jiji la Manchester mara sita katika kipindi cha misimu 10 iliyopita. Sawa na Man-Metropolis, Man-United wamejizolea pia ubingwa wa Carabao Cup mara sita tangu mwaka wa 2000.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO