
Masaibu ya Shujaa yaongezeka vichapo vikizidi Vancouver 7s
Na GEOFFREY ANENE
KENYA Shujaa inaendelea kusikitisha kwenye Raga za Dunia 2022-2023.
Hiyo ni baada ya kuzidiwa maarifa na Fiji na Nice Britain kwenye Kundi C la Vancouver Sevens, Canada, usiku wa kuamkia Jumamosi.
Katika mechi ya kwanza, Shujaa iliongoza 7-0 kupitia kwa mguso wa Herman Humwa ulioandamana na mkwaju kutoka kwa Anthony Omondi ikipoteza 31-12 dhidi ya Fiji. Alvin ‘Buffa’ Otieno alipata mguso pia katika mechi hiyo iliyotanguliwa na Nice Britain kukung’uta Uruguay 45-5.
Kenya ilianza mchuano wa pili vibaya ikinyamazishwa 26-12 na Nice Britain. Ilijipata chini 19-0 kabla ya kupunguza mwanya huo kwa pointi tano baada ya Kevin Wekesa kupata mguso bila mkwaju.
Vijana wa kocha Damian McGrath walihitimisha mchuano na mguso kutoka kwa Edmund Anya ulioandamana na mkwaju. Mabingwa hao wa zamani wa Afrika wameratibiwa kumenyana na Uruguay baadaye Jumamosi usiku. Ni rasmi watawania nafasi za kuorodheshwa nambari tisa hadi 16 (mwisho) kwa sababu hawawezi kuingia robo-fainali kuu.
Source link