Thursday, March 2, 2023
AdvertismentGoogle search engineGoogle search engine
HomeGeneral NewsMathare yafufuka na kuishangaza Gor KPL – Taifa Leo

Mathare yafufuka na kuishangaza Gor KPL – Taifa Leo

Mathare yafufuka na kuishangaza Gor KPL

Mathare yafufuka na kuishangaza Gor KPL

Na CECIL ODONGO

NGUVU mpya Daniel ‘Van Persie’ Otieno jana Jumatano alifunga bao dakika za jioni za kipindi cha pili, Mathare United ilipoilemea Gor 2-1 kwenye mechi ya Ligi Kuu (KPL) iliyosakatwa ugani MISC Kasarani.

Kiungo Otieno alifunga bao hilo dakika ya 84 kwa kuachilia fataki mechi hiyo ikiwa ikionekana kuelekea sare ya 1-1.
Awali bao la Benson Omala dakika ya 65 lilikuwa limefuta lile la dakika ya nane la Douglas Kibet kwa mabingwa hao wa 2008.

Hili lilikuwa bao la 17 la msimu kwa Omala huku Otieno akiwa ameyafunga mabao matano.
Mathare United imekuwa timu ya pili kuchapa Gor msimu huu baada ya KCB.

Wanabenki hao walichapa Gor 1-0 mnamo Januari 4.

Licha ya kupoteza, Gor bado inaongoza KPL kwa alama 37 baada ya mechi 17.

Ushindi huo ulipaisha Mathare hadi mabao 16 kutokana na mechi 16.

Kocha wa Gor Mahia Johnathan McKinstry alisikitikia kichapo hicho huku akisifu Mathare kwa kuonyesha mchezo wa kuridhisha.

“Leo tumepatikana na lazima niseme wapinzani wetu walicheza vizuri. Tulijaribu kurejea mchezoni lakini ikashindikana. Sasa lazima tujisaili na kurekebisha makosa tuliyoyafanya,” akasema McKinstry.

Mwenzake wa Mathare Sam Koko alifurahia ushindi huo akisema walijiandaa vyema kuwakabili Ok’Ogalo.

“Haya ni matunda ya bidii yetu na mazungumzo na wachezaji hawa. Hata baada ya Gor kusawazisha, tuliendelea kuwapa shinikizo na tukapata bao letu,” akasema Kioko.

Katika mechi nyingine, FC Talanta iliongezea Vihiga Bullets masaibu kwa kuichapa 2-1 katika uga wa MISC Kasarani Annex.
Katika mtanange mwingine, Kariobangi Sharks ililemea Wazito 3-1 kwenye uga wa Muhoroni Kaunti ya Kisumu.


Source link

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -spot_img

Most Popular

Home
News
RSS