JUKWAA WAZI: Mbadi, Ichung’wa wageukiana kuhusu ahadi ‘hewa’ ya Ruto
NA WANDERI KAMAU
MNAMO Septemba 2022, Rais William Ruto aliwaahidi Wakenya kwamba angepunguza matumizi ya fedha wizara na idara tofauti za serikali kwa hadi Sh300 bilioni katika bajeti ya kifedha ya mwaka 2023/2024.
Hili ni kwenye mkakati wa “kuwaokoa kutokana na ubadhilifu” ulioendeshwa na serikali ya Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta.
Kwenye ahadi yake, Rais Ruto alisema anafahamu ugumu wa kimaisha unaowakumba Wakenya wengi, hivyo si nia yake kuendelea “kuwazidishia mizigo ya kifedha”.
Miezi mitano baadaye, ingali kudhihirika ikiwa ahadi ya Rais Ruto imetekelezwa au la.
Kulingana na mbunge maalum wa ODM, John Mbadi, Rais Ruto aliwahadaa Wakenya kwani bajeti imepunguzwa kwa Sh14 bilioni pekee, kauli iliyopingwa vikali na Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kitaifa, Kimani Ichung’wa.
Je, ni nani msema kweli?