Sunday, March 5, 2023
AdvertismentGoogle search engineGoogle search engine
HomeUncategorizedMbwa na punda kuchanjwa dhidi ya kichaa cha mbwa – Taifa Leo

Mbwa na punda kuchanjwa dhidi ya kichaa cha mbwa – Taifa Leo

Mbwa na punda kuchanjwa dhidi ya kichaa cha mbwa

Mbwa na punda kuchanjwa dhidi ya kichaa cha mbwa

NA JURGEN NAMBEKA

SERIKALI ya kaunti ya Taita Taveta imeelezea mpango wa kutoa chanjo ya bure kwa mbwa na punda wa kaunti hiyo, ili kuzuia msambao wa ugonjwa wa Rabies (kichaa cha mbwa).

Akizungumza wakati wa kutangaza ushirikiano huo na kampuni ya Brooke East Africa, naibu wa gavana Bi Christine kIlalo alieleza kuwa ni jukumu la kaunti kuhakisha wakazi hawasumbuliwi na ugonjwa huo.

“Tunashukuru sana kampuni ya Brooke kwa kujitolea kutoa chanjo hii. Tunapanga kutoa chanjo, kushughulikia wanyama, kuhamasisha umma na kupunguza idadi ya mbwa. Tutakuwa na uhusiano wa kipidi kirefu kwa ajili ya wakazi wa Taita Taveta,” alisema Bi Kilalo.

Kulingana na mkurugenzi mkuu wa Brooke eneo la Pwani, kampuni hiyo itatoa dosi 5,830 katika awamu ya kwanza ya chanjo zitakazotumika kwa kaunti ndogo nne.