
MCA ataka Mbarire aeleze hatima ya waliopewa likizo
NA GEORGE MUNENE
DIWANI jana Jumanne alitaka maelezo kuhusu hatima ya maafisa wa serikali ya Kaunti ya Embu waliopewa likizo ya lazima mwaka jana na Gavana Cecily Mbarire.
Diwani (MCA) wa wadi ya Ruguru-Ngandori, Muturi Mwombo alisema miezi kadhaa imepita bila habari kutolewa kuhusu iwapo wafanyakazi hao waliosimamishwa kazi kwa madai ya kukosa maadili kazini waliondolewa lawama au la.
Bw Mwombo pia anataka matokeo ya uchunguzi kuhusu suala hilo kufichuliwa kwa Bunge la Kaunti ya Embu na wale waliopatikana na hatia washtakiwe huku walioondolewa lawama wakirudishwa kazini na kufidiwa.
Source link