Thursday, March 2, 2023
AdvertismentGoogle search engineGoogle search engine
HomeGeneral NewsMtiririko wa matukio katika sehemu 11, Onyesho I – Taifa Leo

Mtiririko wa matukio katika sehemu 11, Onyesho I – Taifa Leo

TAMTHILIA: Mtiririko wa matukio katika sehemu 11, Onyesho I

TAMTHILIA: Mtiririko wa matukio katika sehemu 11, Onyesho I

JUMA hili tuangazie mtiririko wa matukio katika sehemu 11, onyesho I.

Mandhari: Ni alasiri, nyumbani kwa Neema, mjini. Neema na mamake wameketi ukumbini, wanashiriki mazungumzo.

Umuhimu wa mandhari – huonyesha wakati (alasiri), mahali (mjini), wahusika (Neema na Sara), hali (ya mazungumzo).

Sara na bintiye Neema wameketi ukumbini huku wakijipepea kutokana na joto. Neema anasema kuwa mji huo una joto jingi utadhani ndio kitovu cha jua (chuku).

Sara anamjuza Neema kuwa hata kule kijijini hali ni ya joto jingi (taswira joto). Hata mimea haina afya. Inanyauka tu. Neema anabashiri kuwa mwakani kuna uwezekano wa kuwa na kipindi kigumu. Neema anagundua kuwa mamake amechoka kutokana na safari ndefu.

Kwa huzuni Sara anazua suala la kutowajibika kwa viongozi “Wamesema tangu tukiwa watoto kwamba maendeleo yaja hadi tumekuwa watu wazima tukajaaliwa watoto na hao watoto nao sasa wameenda zao wala hamna kubwa lililofanyika” (ahadi za uongo). Neema anamsihi mamake asikate tamaa.

Mfanyakazi wa nyumbani kwa Neema, Bela, anawaandalia chakula. Mwanawe Neema, Lemi amechelewa kurudi kutoka shuleni kwa kuwa wana mazoezi ya kujiandaa kwa hafla shuleni (elimu).

Sara anamhimiza bintiye ayafurahie majukumu yake mengi na asichoke kuwafanyia awezalo wanawe aliojaliwa siku za ujana wake kwani watoto ni baraka (malezi).

Neema anahisi kama baba yao (Yona) hakuwapenda kutokana na kugombana na kulalamika kwake walipokuwa watoto na hata kuwashikia mkwaju.

Makala kuendelezwa juma lijalo

Simon Ngige

Alliance Excessive College