Tuesday, February 21, 2023
AdvertismentGoogle search engineGoogle search engine
HomeGeneral NewsMwanasiasa ahofia mali yake kupigwa mnada – Taifa Leo

Mwanasiasa ahofia mali yake kupigwa mnada – Taifa Leo

Mwanasiasa ahofia mali yake kupigwa mnada

Mwanasiasa ahofia mali yake kupigwa mnada

NA DERICK LUVEGA

MWANASIASA mmoja wa kaunti ya Vihiga aliyepoteza katika uchaguzi mkuu uliopita anakabiliwa na hatari ya mali yake kupigwa mnada baada ya kesi yake ya kupinga ushindi wa diwani kutupiliwa mbali kwa gharama.

Hakimu wa Hamisi Melanie Ochieng’ aliamua kwamba Diwani wa wadi ya Banja Collins Ayugu alipwe Sh250,000 na Noah Mbwanga aliyewasilisha kesi ya kupinga ushindi wake.

Bw Mbwanga pia anatarajiwa kuilipa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Sh300,000 kufidia gharama ya tume hiyo katika kesi hiyo.

Diwani Ayugu anasisitiza kwamba ardhi ya Bw Mbwanga iuzwe ili alipwe pesa hizo, jinsi mahakama ilivyoamuru.Jana, diwani huyo alisema amewaagiza madalali kuuza ardhi ya Bw Mbwanga ili aweze kulipwa Sh250,000, kulingana na amri ya Hakimu Ochieng’.

“Kesi hiyo ilitupiliwa mbali kwa gharama ya Sh550,000. Ikiwa mlalamishi hatalipa haraka iwezekanavyo, shamba lake litapigwa mnada,” akasema.

Mawakili wa Bw Mbwanga wanapanga kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo wakisema hawajakubaliana nao.

Kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa wadi ya Banja inaongezea orodha ndefu ya gharama za kesi zinazowakabiliwa walalamishi baada ya kupoteza kesi.

Mamia ya kesi zimewasilishwa katika mahakama za sehemu mbalimbali nchini kupinga matokeo ya uchaguzi wa viti kadhaa katika uchaguzi mkuu wa Agosti 9, 2022.

Kwa mfano, mnamo Februari 9, Jaji David Kemei alidumisha ushindi wa Gavana wa Busia Paul Otuoma na kumwagiza mpinzani wake, Sakwa Bunyasi alipe Sh3 milioni kama gharama za kesi hiyo. Jaji Kemei aliamuru kwamba Bw Otuoma alipwe pesa hizo.


Source link

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -spot_img

Most Popular

Home
News
RSS