
Mwanasoka wa zamani wa Man-United, John O’Shea ateuliwa kuwa kocha msaidizi wa Jamhuri ya Eire
Na MASHIRIKA
BEKI wa zamani wa Manchester United, John O’Shea, ameteuliwa kuwa kocha msaidizi katika timu ya taifa ya Jamhuri ya Eire ambayo sasa inanolewa na mkufunzi Stephen Kenny.
O’Shea, 41, anakuwa kocha msaidizi baada ya kudhibiti mikoba ya kikosi cha chipukizi wa U-21 nchini Eire kwa takriban miaka mitatu iliyopita.
O’Shea ambaye kwa sasa ni mkufunzi wa kikosi cha Stoke Metropolis, alihitimu ukufunzi wa kiwango cha Professional Licence mnamo Disemba 2022. Anatarajiwa kujumuisha majukumu yake mapya yatakayoanza kwa mechi za kufuzu kwa fainali za Euro 2024 na kusimamia pia kikosi cha Stoke Metropolis.
Difenda huyo aliwahi kuchezea Eire mara 118 na ndiye wa tatu katika orodha ya wanasoka wanaojivunia kuwajibikia kikosi hicho mara nyingi zaidi.
“Ni fahari tele kuwa sehemu ya benchi ya kiufundi ya timu ya taifa ya Eire,” akasema O’Shea aliyekuwa sehemu ya kikosi kilichonogesha fainali za Euro 2012 na 2016.
Akivalia jezi za Man-United, sogora huyo aliwahi kunyanyua mataji matano ya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) na moja la Klabu Bingwa Ulaya (UEFA).
Jamhuri ya Eire wamepangiwa kuanza mechi za kufuzu kwa fainali za Euro 2024 kwa mechi ya nyumbani dhidi ya Ufaransa mnamo Machi 27, 2023, siku tano baada ya kuwa wenyeji wa Latvia katika pambano la kirafiki jijini Dublin.
TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO
Source link