Friday, March 3, 2023
AdvertismentGoogle search engineGoogle search engine
HomeGeneral NewsNCPB yakumbwa na upungufu wa mahindi licha ya kupandisha bei ya mazao...

NCPB yakumbwa na upungufu wa mahindi licha ya kupandisha bei ya mazao ya wazalishaji – Taifa Leo

NCPB yakumbwa na upungufu wa mahindi licha ya kupandisha bei ya mazao ya wazalishaji

NCPB yakumbwa na upungufu wa mahindi licha ya kupandisha bei ya mazao ya wazalishaji

NA BARNABAS BII 

HALMASHAURI ya Kitaifa ya Nafaka na Mazao (NCPB) imenunua magunia 43,000 ya mahindi pekee ya thamani ya Sh241 milioni huku ikikabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa viwanda vya kusaga unga pamoja na wafanyabiashara wa kibinafsi.

Halmashauri hiyo inakabiliwa na changamoto kutoka kwa wakulima katika eneo la Kaskazini mwa Bonde la Ufa, linalozalisha chakula kwa wingi nchini, hata baada ya kuongeza bei ya ununuzi kutoka Sh5,100 hadi Sh5,600 na kuwalipa bila kuchelewa.

Hii inatokana na ushindani mkali kutoka kwa viwanda vya unga na wafanyabiashara wanaonunua gunia la kilo 90 kwa Sh6,200.

“Tumenunua karibu magunia 43,000. Vituo vyetu viko wazi na tunahimiza wakulima kuwasilisha mazao yao,” alisema Meneja wa NCPB Kaskazini mwa Bonde la Ufa, Bw Gilbert Rotich.

Uchunguzi wa Taifa Leo ulipata kuwa foleni za wakulima wanaowasilisha mazao yao kwa mabohari ya Eldoret, Kitale, Moi’s Bridge na Ziwa zimepungua.

Mkurugenzi wa NCPB, Bw Joseph Kimote, alirai wazalishaji kutumia vyema fursa hii ya bei nafuu kuwasilisha mazao yao katika bohari lolote kote nchini.

“Vituo vyetu viko wazi na tunataka mje mfanye biashara nasi. Hakuna kucheleweshwa tena kwa malipo ya wakulima kwa sababu sasa tunawalipa kupitia M-Pesa,” akaeleza Bw Kimote.

Halmashauri hiyo imenunua magunia 50,000 ya mahindi kufikia sasa.


Source link

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -spot_img

Most Popular

Home
News
RSS