Saturday, March 4, 2023
AdvertismentGoogle search engineGoogle search engine
HomeGeneral NewsNdugu waagizwa wamalize kesi nje ya korti – Taifa Leo

Ndugu waagizwa wamalize kesi nje ya korti – Taifa Leo

Ndugu waagizwa wamalize kesi nje ya korti

Ndugu waagizwa wamalize kesi nje ya korti

NA RICHARD MUNGUTI

MBUNGE wa zamani James Ndung’u Gethenji na ndugu yake wanaozozana kuhusu udhibiti wa mali ya familia ya thamani ya Sh20 bilioni wameagizwa na mahakama wasuluhishe kesi hiyo nje ya korti.

Hakimu mwandamizi mahakama ya Milimani Bernard Ochoi aliwashauri Bw Gitahi Gethenji na Ndung’u wasuluhishe mzozo baina yao nje ya korti.

Bw Ochoi alimtaka wakili Prof George Wajackoya anayemwakilisha Gitahi afanikishe mazugumzo baina ya ndugu hao.

Ripoti kuhusu mashauri hayo itawasilishwa kortini Juni 14, 2023.

Wakili Willis Otieno anayemwakilisha Ndung’u katika kesi ya kuhatarisha amani katika mtaa wa Kihingo alisema “wako tayari kusuluhisha kesi hiyo.”

“Tumeandika barua kadhaa tukieleza azma ya kutaka kusuluhisha kesi hii Gitahi ndiye amekuwa na ugumu wa moyo,” Bw Otieno alisema.

Kiongozi wa mashtaka Bw James Gachoka alisema kesi aliyoshtakiwa Ndung’u pamoja na Josiah Augo Otieno, Godfrey Ochieng Okello, Kennedy Ochieng Asewe na Shadrack Ouma Okonji ya kuvuruga amani haipasi kuendelea ilhali mlalamishi (Gitahi) anaweza akaifutilia mbali.

“Ndugu hawa wamefaulu kusuluhisha kesi zilizokuwa katika mahakama kuu kuhusu udhibiti wa mali hiyo ya familia. Pia wanaweza kusuluhisha kesi hii,” Bw Gachoka alimweleza hakimu.

“Hii kesi nitaitengea siku nyingine ya kusikilizwa lakini nawapa fursa ndugu hawa wawili wakutane wasuluhishe kesi hii,” alisema Bw Ochoi.

Akitoa ushahidi katika kesi hiyo mfanyakazi wa kampuni ya Wells Fargo inayolinda mtaa huo wa kifahari wa Kihingo Village Waridi Gardens Bw Gabriel Kamau Lumia alisema hakumuona James Ndung’u Gethenji akitoa vurugu mnamo Oktoba 16,2019.

“Sikumuona Ndung’u ambaye ni mwenyekiti wa kampuni ya Kihingo wakati wa ghasia hizo,” bw Lumia alisema alipohojiwa na Bw Otieno.

Mahakama ilifahamishwa walinzi wa Wells Fargo walitimuliwa mbio na afisa aliyeajiriwa na Kihingo Bw Frank Mutegi kusimamia usalama.