Saturday, March 4, 2023
AdvertismentGoogle search engineGoogle search engine
HomeGeneral NewsNigeria ni mfano bora kuwa mtu mui hatimaye huwa mwema – Taifa...

Nigeria ni mfano bora kuwa mtu mui hatimaye huwa mwema – Taifa Leo

WANDERI KAMAU: Nigeria ni mfano bora kuwa mtu mui hatimaye huwa mwema

WANDERI KAMAU: Nigeria ni mfano bora kuwa mtu mui hatimaye huwa mwema

NA WANDERI KAMAU

MTU anapofanya vizuri ikilinganishwa na vitendo vyake vya awali, anafaa kupongezwa kwa kuimarisha vitendo ama mwelekeo wake.

Ni sawa na mwanafunzi anayeboresha matokeo yake ya mtihani ikilinganishwa na hapo mbeleni.

Badala ya kukashifiwa, mwanafunzi huyo anafaa kupongezwa ili atie bidii zaidi masomoni mwake. Hiyo ndiyo taswira iliyopo kwa sasa nchini Nigeria, kufuatia uchaguzi uliofanyika Jumamosi wiki iliyopita.

Baada ya karibu wapigakura milioni 25 kati ya milioni 90 waliosajiliwa kushiriki katika uchaguzi huo, Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi (INEC) ilimtangaza Bola Tinubu wa chama tawala cha All Progressives Congress (APC) kuwa mshindi wa urais.

Aliwashinda wapinzani wake wakuu; Atiku Abubakar wa chama cha Folks’s Democratic Get together (PDP) na Peter Obi wa Labour Get together. Ingawa Upinzani umeeleza kutoridhishwa na matokeo hayo, hii ni taswira ya kipekee inayoshuhudiwa nchini Nigeria.

Ni mara ya kwanza uchaguzi kufanyika nchini humo bila visa vya ghasia kuripotiwa.

Huu ni mwelekeo mzuri na wa kuridhisha sana katika taifa ambalo halikujua maana halisi ya demokrasia hadi 1999.

Nigeria ilikuwa chini ya tawala tofauti za kijeshi tangu ilipojinyakulia uhuru wake kutoka kwa Uingereza mnamo 1960.

Watawala hao wa kijeshi walitumia mamlaka yao kulipora taifa hilo ili kujifaidi wao wenyewe.

Hata hivyo, uchaguzi wa Jumamosi ni ishara tosha kuwa taifa hilo linaendelea kukuza demokrasia yake.


Source link

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -spot_img

Most Popular

Home
News
RSS