
VITUKO: Nyumbani kwa Gundogan wanahesabu siku tu za kukaribisha kifungua mimba
IMEKUSANYWA NA CHRIS ADUNGO
KIUNGO mzoefu wa Manchester Metropolis na timu ya taifa ya Ujerumani, Ilkay Gundogan, amesema ni siku za kuhesabu tu zimesalia kabla ya mkewe Sara Arfaoui kumwangushia toto la kiume.
Gundogan, 32, alitumia mtandao wa Instagram kufichua hali ya ujauzito wa mkewe, 27, kwa kupakia emoji ya moyo iliyokolezwa kwa samawati.
Akaandika chini yake: “Tunakusubiri kwa hamu kubwa mtoto wetu Gundo Jr.”
Kwenye video fupi iliyopakiwa pia na sogora huyo wa zamani wa Borussia Dortmund, Sara alikuwa amevalia rinda jeusi huku amekamatwa tumboni na dume lake.
Baadaye walishikana mikono huku Gundogan, aliyejaa raha tele, akimbusu mkewe shavuni na kwenye paji la uso.
Gundogan alianza kumtambalia Sara kimapenzi mnamo 2018, na alimvisha pete ya ndoa mnamo Mei iliyopita jijini Roma, Italia.
Source link