Friday, February 24, 2023
AdvertismentGoogle search engineGoogle search engine
HomeGeneral NewsOsimhen asaidia Napoli kupepeta Eintracht Frankfurt 2-0 katika pambano la UEFA nchini...

Osimhen asaidia Napoli kupepeta Eintracht Frankfurt 2-0 katika pambano la UEFA nchini Ujerumani – Taifa Leo

Osimhen asaidia Napoli kupepeta Eintracht Frankfurt 2-0 katika pambano la UEFA nchini Ujerumani

Osimhen asaidia Napoli kupepeta Eintracht Frankfurt 2-0 katika pambano la UEFA nchini Ujerumani

Na MASHIRIKA

VICTOR Osimhen alifunga bao lake la 20 msimu huu na kusaidia Napoli kutandika Eintracht Frankfurt 2-0 katika mchuano wa mkondo wa kwanza wa hatua ya 16-bora ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) mnamo Jumanne usiku nchini Ujerumani.

Khvicha Kvaratskhelia wa Napoli alipoteza mkwaju wa penalti kabla ya Osimhen kuwaweka waajiri wake kifua mbele kwa kukamilisha krosi ya Hirving Lozano katika dakika ya 40.

Frankfurt walijipata matatani zaidi katika dakika ya 58 baada ya mshambuliaji wao tegemeo, Randal Kolo Muani, kuonyeshwa kadi nyekundu. Tukio hilo liliwachochea Napoli kuteremkia wenyeji wao na wakafunga bao la pili kupitia kwa Giovanni di Lorenzo katika dakika ya 65.

Ushindi huo uliwaweka Napoli katika nafasi nzuri ya kutinga robo-fainali kadri wanavyosubiri kunogesha mechi ya marudiano nchini Italia mnamo Machi 15, 2023.

Napoli wanaonolewa na kocha Luciano Spalletti wamekuwa katika fomu nzuri zaidi muhula huu na wanajivunia pengo la alama 15 kati yao na nambari mbili Inter Milan kileleni mwa jedwali la Ligi Kuu ya Italia (Serie A).

Miamba hao wanaopigiwa upatu wa kutwaa taji la Serie A kwa mara ya kwanza tangu 1989-90, walishuka dimbani dhidi ya Frankfurt wakijivunia kushinda mechi tano mfululizo katika mashindano yote.

Huku Napoli wakiwapiku Liverpool, Ajax na Rangers na kudhibiti kilele cha Kundi A, Frankfurt waliambulia nafasi ya pili nyuma ya Tottenham Hotspur katika Kundi D lililojumuisha pia Sporting Lisbon na Olympique Marseille.

Sawa na Frankfurt waliopepeta Werder Bremen 2-0 katika mechi yao iliyopita ya Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga), Napoli nao walijibwaga ulingoni Jumanne usiku wakiwa na kiu ya kuendeleza ubabe uliowapa ushindi wa 2-0 dhidi ya Sassuolo katika Serie A.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO


Source link

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -spot_img

Most Popular

Home
News
RSS