Saturday, February 25, 2023
AdvertismentGoogle search engineGoogle search engine
HomeGeneral NewsRuto aendelea kufyeka watu walioteuliwa na Uhuru serikalini – Taifa Leo

Ruto aendelea kufyeka watu walioteuliwa na Uhuru serikalini – Taifa Leo

Ruto aendelea kufyeka watu walioteuliwa na Uhuru serikalini

Ruto aendelea kufyeka watu walioteuliwa na Uhuru serikalini

NA CHARLES WASONGA

RAIS William Ruto ameendelea kuwatunuku wandani wake wa kisiasa kwa kuwateua kushikilia nyadhifa za uongozi katika mashirika mbalimbali ya serikali.

Wa hivi punde kuzawadiwa ni aliyekuwa mgombeaji wa kiti cha ubunge cha Ainamoi Sylvanus Maritim, mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Ukoo wa Talai Kasisi James Bassy na aliyekuwa mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Myoot Meja Mstaafu John Sei.

Kupitia tangazo kwenye gazeti rasmi la serikali toleo la Ijumaa, Februari 24, 2023, Rais Ruto amemteua Bw Maritim kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) kwa kipindi cha miaka mitatu. Uteuzi wa mwenyekiti wa sasa Profesa Fredrick Owino, aliyeteuliwa na Rais mstaafu Uhuru Kenyatta,  umefutuliwa mbali.

Bw Maritim alishindwa na mbunge wa sasa wa Ainamoi Benjamin Lang’at katika mchujo wa chama cha United Democratic Alliance (UDA) uliofanyika Aprili 2022.

Nao Kasisi Bassy na Mzee Seii wameteuliwa kuwa wanachama wa Baraza la Kusimamia Kituo cha Kitamaduni Nchini (Kenya Cultural Centre Council) na watahudumu kwa miaka miwili.

Kasisi Bassy, kama mwenyekiti wa baraza la wazee wa Talai ndiye alioongoza hafla ya kumtawaza Rais Ruto kuwa kinara wa jamii ya Kalenjin badala ya mwenyekiti wa Kanu Gideon Moi.

Rais Ruto pia amefutilia mbali uteuzi wa Wanjiku Wakogi kama Katibu wa Kamati ya Ushauri wa Mashirika ya Serikali (SCAC) na kumteua Muyumba Simmon Indimuli ambaye atashikilia wadhifa huo kwa miaka mitatu.

Kiongozi wa taifa pia alifanya mabadiliko katika Mamlaka ya Soko la Hisa (CMA) kwa kumfuta kazi mwenyekiti wake Nick Nesbitt aliyeteuliwa na Bw Kenyatta na kumteua ugas Mohamed katika nafasi yake.

Aidha, Rais amewateua Natasha Awuor Aduwo, Elena Natalia Pellegrini, Meshack Moses Kiprono, Gibson Kimani Maina na  Michael Bowen. Watano hawa wamechukua nafasi za; Natasha Awuor Aduwo, Elena Natalia Pellegrini, Meshack Moses Kiprono, Gibson Kimani Maina na Michael Bowen.


Source link

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -spot_img

Most Popular

Home
News
RSS