
Ruto asukuma magavana kufadhili miradi
NA VALENTINE OBARA
MAGAVANA watalazimika kutenga fedha zaidi za maendeleo iwapo wangependa serikali ya kitaifa isaidie kufanikisha miradi ya kaunti zao.
Alipokuwa Lamu wikendi, Rais William Ruto (pichani), alisema alikutana na magavana wa kaunti za Pwani wakakubaliana serikali ya kitaifa itakuwa ikiongeza fedha pale ambapo kaunti imewekeza kwa maendeleo.
Kaunti nyingi zimekuwa zikilaumiwa kwa kutumia kiasi kikubwa cha fedha kugharimia mishahara na mahitaji mengine, tofauti na ufadhili wa miradi ya maendeleo.
Source link