Saturday, February 25, 2023
AdvertismentGoogle search engineGoogle search engine
HomeGeneral NewsSerikali kuwapa fidia wahasiriwa wa mikasa ya moto Watamu – Taifa Leo

Serikali kuwapa fidia wahasiriwa wa mikasa ya moto Watamu – Taifa Leo

Utalii: Serikali kuwapa fidia wahasiriwa wa mikasa ya moto Watamu

Utalii: Serikali kuwapa fidia wahasiriwa wa mikasa ya moto Watamu

NA ALEX KALAMA 

WAZIRI wa Utalii humu nchini Peninah Malonza amesema kuwa serikali itawafidia wahasiriwa walioathirika na mkasa wa moto ulioteketeza jumla ya hoteli tatu katika eneo la Watamu, Kaunti ya Kilifi.

Waziri huyo amedokeza kuwa licha ya wafanyibiashara hao kukosa bima ya biashara wanazoendeleza, serikali imeweka mikakati ya kuwapa msaada wa kuendeleza biashara zao hata baada ya mkasa huo.

Akizungumza katika eneo hilo, Malonza  amedokeza kuwa tayari serikali inashirikiana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha kuwa hoteli zilizoathirika na mkasa huwo zinajengwa upya ili kuendeleza shughuli za kitalii eneo hilo.

“Watu wa bima wanaendelea kushughulika hoteli iweze kurudi mahali ilikuwa upande wa serikali tutashirikiana nao,pia kuna vibanda vya akina mama waliokuwa wanauza pale nje lakini vikateketea. Hao akina mama hawako kwa hizi ‘affiliation’ za hoteli nitaanza nao siku ya leo nihakikishe nimewaachia kitu kidogo waweze kuanza ujenzi wa hivyo vibanda mara moja,” alisema Bi Malonza.

Kwa upande wake mbunge wa Kilifi Kaskazini Owen Baya amekilaani vikali kitendo cha wizi wa mali wakati wa mkasa huo huku akiwataka wakazi wa eneo hilo kuzingatia umuhimu wa sekta ya utalii katika eneo hilo.

“Wakati wa uokoaji watu walienda wakapora watalii na wamesema sasa wanafikiria kujitoa Watamu wawe hawaleti tena wageni, Alipituri isipoleta wageni hapa kweli kutakuwa na wageni hapa Watamu? Manake hii Watamu ndio peke yake iko na watalii. Malindi hakuna watalii wengi hivyo tuchunge kwa sababu utalii ndiyo raslimali yetu, ndiyo kahawa yetu, ndiyo chai yetu,” akasema Bw Baya.

Ziara ya viongozi hao inajiri baada ya mkasa wa moto ulioaminika kusababishwa na hitilafu za nguvu za umeme eneo hilo na kuteketeza hoteli za Barracuda, Mapango na Mbuyu Lodge juma hili.


Source link

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -spot_img

Most Popular

Home
News
RSS