
Uhaba wa maji mateso tele kwa wakazi vijijini
NA KALUME KAZUNGU
WAKAZI wa Kizingitini, Kaunti ya Lamu, wamelalamikia uhaba wa maji kutokana na kiangazi kinachoendelea kushamiri.
Wakazi hao ambao hutegemea maji ya mvua yaliyohifadhiwa, wameomba serikali ya kaunti kuanzisha usambazaji vijijini mwao.
“Mara kadhaa tumejionea mitaro ikichimbwa ya kuweka mabomba ya maji eneo hili la Lamu Mashariki. Waharakishe kutuunganisha na maji ya mfereji ili kuizika hii taabu ya maji kwenye kaburi la sahau,” akasema Bw Omar Shee.
Source link