
TIBA NA TABIBU: Wakenya wapokea chanjo kudhibiti kipindupindu
NA WANGU KANURI
WAKENYA zaidi ya milioni mbili wamepokea chanjo dhidi ya ugonjwa wa kipindupindu.
Chanjo hii itapewa watu wote walio na umri wa mwaka mmoja. Watu wanashauriwa kutokunywa maji kwa muda wa dakika tano baada ya kupokea chanjo.
Kwa mujibu wa mkuu wa mpango wa kutoa chanjohiyo katika Wizara ya Afya, Dkt Lucy Mecca, kuna matumaini ya kuwachanja Wakenya wengi kupitia mpango huo.
Kaunti zinazolengwa kwenye mpango huo ni pamoja na Nairobi, Garissa, Wajir na Tana River huku maafisa wa afya wakiwapatia Wakenya chanjo hii manyumbani kwao, shuleni na hata sokoni haswa katika maeneo ambayo ugonjwa huu umekithiri.
Oktoba 2022, visa zaidi ya 4,600 vilirekodiwa huku watu 84 wakifariki dunia kutokana na ugonjwa huo. Wizara ya Afya ilisema kuwa , ugonjwa wa kipindupindu ulianza kurekodiwa nchini Machi 2022.
Hali duni ya afya katika mikahawa na vioski vya kupika vyakula inachangia kuzuka na kuenea kwa ugonjwa huu katika baadhi ya kaunti.
Source link