Sunday, March 5, 2023
AdvertismentGoogle search engineGoogle search engine
HomeUncategorizedWanafunzi wa Sekondari ya Msingi pia wapatiwe basari, Seneta apendekeza – Taifa...

Wanafunzi wa Sekondari ya Msingi pia wapatiwe basari, Seneta apendekeza – Taifa Leo

Wanafunzi wa Sekondari ya Msingi pia wapatiwe basari, Seneta apendekeza

Wanafunzi wa Sekondari ya Msingi pia wapatiwe basari, Seneta apendekeza

NA MARY WANGARI

WANAFUNZI wa Seknodari ya Msingi (JSS) huenda wakanufaika vilevile kutokana na basari endapo pendekezo lililotolewa na Seneta wa Kaunti ya Kiambu, Karungo wa Thangwa, litaidhinishwa kuwa sheria.

Kupitia pendekezo lake ambalo bado halijawasilishwa rasmi Bungeni ili kujadiliwa, Bw Thang’wa ametoa wito kwa Bunge la Kitaifa kufanyia marekebisho Sheria zinazohusu Hazina ya Serikali ya Kitaifa kuhusu Ufadhili wa Masomo (NG-CDF) na Basari za Kaunti ambazo kwa sasa haziwajumuishi wanafunzi wa JSS.

Pendekezo hili limejiri wakati ambapo Wizara ya Elimu inajitahidi kutekeleza kikamilifu Mtaala Mpya wa Elimu (CBC) huku ikibainika kuwa baadhi ya wazazi na walezi wanafanya kila juhudi kuwaepusha watoto wao kujiunga na sekondari za msingi.

Awamu ya kwanza ya Sekondari za Msingi zinazojumuisha Gredi 7, Gredi 8 na Gredi 9 ilianza rasmi mwanzoni mwa Februari huku wanafunzi wa Gredi 6 waliofanya mtihani wa Tathmini ya Shule ya Msingi Nchini (KPSEA) wakijiunga na Gredi 7.

Akizungumza na Taifa Jumapili, Seneta Thangwa alihoji kuwa licha ya serikali kupiga hatua katika utekelezaji wa CBC ikiwemo kuazishwa kwa JSS, mzigo wa karo ungali changamoto kuu kwa Wakenya maskini.

“Licha ya juhudi hizi, gharama ya elimu ingali changamoto kuu kwa familia, hasa kutoka jamii maskini. Hapa ndipo mipango ya basari inapokujia. Basari hutoa msaada kwa kifedha kwa wanafunzi maskini kwa kuwasaidia kuendeleza elimu yao na kufikia upeo wao kikamilifu,” alihoji Seneta Thangwa.

“NGCDF na basari kadhaa za kaunti hutoa basari kwa wanafunzi katika viwango vya sekondari na vyuo. Hata hivyo, sheria hizo kwa sasa hazijumuishi wanafunzi katika JSS. Huku Seknodari za Msingi zikianzishwa, ni muhimu kwa sheria zinazosimamia NGCDF na basari za kaunti kufanyiwa marekebisho ili kujumuisha wanafunzi hawa kama miongoni mwa wanaofadhiliwa,” alieleza.

Kwa kupanua upeo wa mipango ya basari kwa JSS, wanafunzi kutoka familia maskini watapata raslimali muhimu kama vile sare na vitabu hivyo kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika elimu yao, anafafanua Bw Thangwa.

Kando na kutoa ufadhili wa karo, muundasheria huyo anapendekeza kuwa sheria za CDF na Basari za Kaunti zifanyiwe marekebisho ili kujumuisha sare na vitabu vilevile kwa wanafunzi wa JSS.

“Hii itasaidia kupunguzia familia mzigo kwa kuwaruhusu kujishughulisha na mahitaji mengine muhimu,” anasema.

“Isitoshe, kwa kujumuisha wanafunzi wa JSS katika mipango ya basari, tunaweza kuhakikisha kuwa wanapokea msaada wanaohitaji ili kujiendeleza kutoka elimu ya msingi hadi sekondari. Hii itasaidia kuboresha nafasi zao za ufanisi na kuongeza ubora wa elimu nchini kwa jumla.”

“Uzinduzi wa JSS nchini unatoa fursa kwa taifa kuwekeza zaidi katika sekta ya elimu nchini,” anasema.

mwnyambura@ke.nationmedia.com


Source link

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -spot_img

Most Popular

Home
News
RSS