
Watalii watatu wajeruhiwa katika mkasa wa moto hotelini Watamu
NA ALEX KALAMA
RAIA watatu wa kigeni wamejeruhiwa vibaya katika mkasa wa moto uliounguza hoteli tatu eneo la Watamu kaunti ya Kilifi.
Watatu hao ambao ripoti za awali zinasema ni Wataliano, walikuwa wamekodi vyumba vya kuishi katika hoteli ya Mubuyu Lodge iliyoko Watamu, inasemekana walikuwa wamelala wakati moto huo ulipozuka na kuunguza hoteli hiyo waliyokuwa ndani na kisha baadaye moto huo uliruka na kuteketeza nyingine mbili ikiwemo hoteli ya Barracuda pamoja na ile ya Mapango.
Majeruhi wamepelekwa Hospitali ya kaunti-ndogo ya Malindi. Ingawa hivyo, mmoja anahamishwa kupelekwa Mombasa kwa matibabu spesheli.
Akizungumza na Taifa Leo kwa njia ya simu kamanda wa polisi eneo la Malindi John Kemboi amesema kwa sasa haijabainika kilichosababisha moto huo ila wanaendelea kukusanya taarifa na watakapokamilisha ataweka wazi ripoti kamili.
Source link